ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

SIASA

WATU 922,000 WALIHAMA MAKWAO MWAKA 2016 NCHINI DRC

By

on

                         Watu 922,000 walihama makwao mwaka 2016 nchini DRC

Idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao kutokana na mzozo ndani ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo mwaka uliopita, ilikuwa ni ya juu kuliko idadi ya watu waliohama makwao nchini Syia na Iraq.

Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ilishuhudia ongezeko la watu 922,000 waliohama kutokana na mzozo mwaka uliopita, ikilinganishwa na watu 824,000 waliohama nchini Syria na 659,000 nchini Iraq.

Watafiti kutoka baraza ya wakimbizi nchini Norway NRC walihesabu zaidi ya watu 922,000 ambao walilazimika kukimbia makwao ndani mwa DRC mwaka 2016.

Katibu mkuu wa NRC Jan Egeland aliiambia BBC kuwa ni jambo la kushangaza kuwa sio Syria au Iraq zilizo na wahamiaji wengi.

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close