ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

WANAFUNZI WAWILI WA SHULE YA MSINGI CHIKOMO WILAYANI TUNDURU WAFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI.

By

on

Na Steven Augustino, Tunduru

WANAFUNZI wawili wa Shule ya msingi Chikomo katika kata ya Mbesa Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na Kifusi wakati wakichimba mchanga.

Ajali hiyo ilitokea Agost 15 mwaka huu na kwamba katika tukio hilo wanafunzi hao walikuwa wakichimba mchanga kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa darasa katika Shule yao.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Kamishina Mwandamizi wa Polisi Jemini Mushi aliwataja wanafunzi hao kuwa Sofia Ngongi na Semen Selemani  wanaosoma darasa la Tatu Shuleni hapo.

Akizungumzia tukio hilo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Omary Melle alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9.20 baada ya wanafunzi hao kutoka madarasani baada ya muda wa masomo kwisha.

Alisema shule yake imekuwa ikiwatumia wanafunzi wa shule hiyo kusomba mchanga kutokana na wawazi na walezi wa watoto wanaosoma katika Shule hiyo kugoma kufanya kazi za kujitolea ili kufanikisha ujenzi wa darasa shuleni hapo.

Wakisimulia mkasa huo afisa mtendaji wa Kata ya mbesa Raso Kundete na diwani wa kata hiyo Abdul Mfaume walisema kuwa baada ya tukio hilo wanafunzi hao walipiga kelele kwa ajili ya kuomba msaada kwa watu wazima ambao waliende kuoko miili hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa Shile hiyo Mkape Hasan Nasoro alidhibitisha kutolewa kwa mamlaka kwa walimu hao kuwatumia wanfunzi hao kubeba mchanga huo ili kuharakisha ujenzi wa darasa hilo.

Wakiongea kwa nyati tofauti baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho waliwatuhumu walimu hao kuwa wamekuwa na tabia za kuwatumikisha watoto wao jambo ambalo limekuwa likiwakesha.

Akifafanua taarifa hiyo mweneyekiti wa serikali ya Kijiji cha Chikomo Mitawa Adam alisema kuwa wanafunzi hao walianza kubebeshwa mchanga huo bila kutoa taarifa yoyote kwa viongozi.

Alisema wananchi wa kijiji chake ni wasikivu na ndiyo maana walikubali kujitolea kufyatua matofari 135, 000 ambayo kwa sasa yanatumiwa kwa ajili ya ujenzi wa darasa hilo.

Mganga aliyeifanyia uchnguzi miili ya Wanfunzi hao Dkt. Andreas Ndunguru alisema kuwa chanzo cha kifo hicho kilitokana na wanafunzi hao kukosa hewa baada ya kufunikwa na kifusi cha udongo huo.

Mwisho

 

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close