ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

SIASA

Wabunge wa upinzani waendelea kupata vitisho nchini Uganda

By

on

Nchini Uganda, sula ambalo limekua gumzo ni lile la marekebisho ya Katiba kuhusu ukomo wa umri wa rais Museveni kuendelea kuwania kiti cha urais nchini humo.

Rasimu ya marekebisho ya Katiba itamruhusu Museveni ambaye yuko madarakani kwa zaidi ya 30 miaka, kuwania muhula mwingine mnamo mwaka 2021.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI mjini Kampala, Charlotte Cosset, wabunge wa upinzani wanaendelea kukabiliwa na vitisho na hata mashambulizi ya kimwili. Siku ya Jumanne, rasimu ya ya marekebisho ya Katiba iliwasilishwa bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa kwanza. Hata hivyo wabunge wachache wa upinzani ndio walikua walishiriki kikiao hicho,

Nakala iliwasilishwa rasmi bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza. Lakini licha ya idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala na washirika wake, viti vya wabunge wa upinzani vilisali tupu. Edson Kafuuzi, mmoja wa wanaharakati wa marekebisho ya Katiba amesema upinzani haipaswi kubeba lawama.

“Wao hawako hapa kwa sababu wamesimamishwa au wamechukua uamuzi wa kujitenga nasi. Kwa hiyo hali hii haina uhusiano na vitisho. Hata kwa sisi wasaidizi wa muswada huu tunapokea vitisho. Tatizo pekee ambalo ninaona ni kwamba wenzetu katika upinzani walianza kile walichokiita upinzani kama fomu ya maandamano lakini ni kuchochea vurugu. »

Katika muda wa wiki moja, gruneti zilirushwa mbele ya makazi ya wabunge watatu wa upinzani. Jumanne asubuhi nyumbani kwa Bobi Wine, mwimbaji maarufu ambaye hivi karibuni aliingia katika siasa alikumbwa na hasara kubwa baada ya kushambuliwa kwa gruneti .

Mwimbaji huyo maarufu amesema hashangazwi na mashambulizi haya.

«Kabla ya hapo nimekuwa nikipokea ujumbe usiojulikana unanionya mimi kuacha kupinga kuondolewa kwa kikomo cha umri au nitauawa. Haya yote yamekusudiwa kwa maoni yangu kwa kunitisha na familia yangu. Lakini ninawaambia watu hao kwamba sijalitishio siogopi kubadili nia yangu ya kulinda Katiba. »

Kamati ya kisheria sasa ina siku 45 ili kuwasilisha upya nakala hii bungeni kwa minajili ya kujadiliwa

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close