ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

ELIMU

VIJANA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KULETA MAENDELEO YA BARA LA AFRIKA

By

on

NaHumphrey Shao,

Vijana barani Afrika wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika  kueleta Maendeleo hili kufikia malengo hasa
katika kipindi hiki cha mapinduzi ya Teknolijia na Viwanda.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya Wanawake Jinsia na Watoto, Dk .Hamisi Kigwangalla alipokuwa akifungua kongamano la Vijana barani Afrika lililoandaliwa na
Tasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais Kigwangala amesema kuwa mara zote vijana wanapokusanyika na kujadili maendeleo ya bara la Afrika ni muhimu sana kwani leo vijana ndio wadau wakubwa katika swala zima la maendeleo ya bara lao  .

 “inaeleweka
kabisa ukuaji wa bara la Afrika unategemea vijana ndio maana ajenda ya 2063 inahusisha ubunifu , Nishati , utamaduni na swala zima la siasa safi  kama serikali tunawahimiza vijana kujitambua
nakuwawezesha  kufikia malengo hili kuweza kupambana na vikwazo vinavyo wakabili” amesema Kigwangala.

Ameongeza kuwa vijana wanatakiwa kutambua vikwazo vinavyo wakabili kama fursa ya kujipatia maendeleo kwa kutatua vikwazo hivyo kwa ajili ya maendeleo ya vijana wa kesho.

Amesema mjadala wa leo sio tu kwa ajili ya Vijana bali ni kwa ajili ya maendeleo ya bara la Afrika kwa kuwa na sera zitakazowawezesha vijana.

 

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close