ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

ELIMU

UKOSEFU WA MAJI WADAIWA KUWA KIKWAZO CHA MASOMO KWA WATOTO WAKIKE

By

on

Na Steven Augustino, Tunduru

 

 IMEELEZWA kuwa Ukosefu wa maji safi na salama katika baadhi ya shule za msingi na sekodnari zilizopo kztika  Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, kumeendelea kuwatesa wanafunzi hasa wasichana ambao wamekuwa wakitembea umbali wa hadi kilometa nne kutafuta huduma hiyo.

 

Aidha mwandishi wa habari hizi pia alishuhudia baadhi ya madarasa yakiwa yamegeuzwa mabweni kwa ajili ya watoto wa kike ambao wanatokea katika maeneo ya Vijiji jirani kwa ajili ya kuwakinga na vikwazo vya wanaume ambao kutokana na kuishi hapo bado wanakabiliwa na tatizo la maji.

 

Hayo yalibainishwa na Wanafunzi wa Shule hiyo wakati walipo tembelewa na Mwaandishi wa habari hii shuleni hapo na kwamba ukosefu wa huduma hiyo umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa anguko kwa watoto wa kike.

 

Shule hiyo yenye wanafunzi 269 wakiwamo wavulana 178 na wasichana 98 hutumia maji ya Visima Vifupi kutoka katika mto uliopo katika eneo hilo jambo ambalo lilidaiwa kuwa ni kikwazo kwa mienendo ya masomo kwa wanafunzi hao kuhelewa vipindi inapo tokea masomo yanananza wakati wao wakiwa wametumwa kwenda kuchota maji hayo.

 

Walisema pamoja na kikwazo hicho ya kukosa masomo hayo lakini tatizo kubwa zai lipo kwa watoto wakike ambao mbali na maamuzi ya kutengwa kwa baadhi ya madarasa hayo kwa ajili ya kulalal wanafunzi hao wakiwemo watoto wa kike kwa lengo la kuwakinga na wanaume ili wamalize masomo lakini wengi wa mabinti hao wamekuwa wakipata ujauzito kwa kushawishiwa kufanya mapenzi pindi wanapo kwenda kuchota maji.

 

 

Diwani wa kata ya Mrumba  Msenga Said alikiri kuwepo kwa kadhia hiyo na kwamba awali kulikuwa na Bomba la maji ya kupampu shuleni hapo lakini toka liharibike hali imekuwa mbaya zaidi

 

Msinga aliendelea kufafanua kuwa kutokana na kadhia hiyo Baadhi ya wanafunzi shule ya sekondari marumba, ambao wamekuwa wakikumbana matukio yanayosababisha baadhi ya wao kutomaliza masomo, yakiwemo kupata ujauzito wa watoto wa kike  wanapokuwa katika harakati za kusaka huduma hiyo.

 

Mkuu wa wilaya ya tunduru, juma omera amekiri kuwapo kwa tatizo la maji lakini akasema serikali inachukua hatua ili kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na watu.

 

Alisema pamoja na Serikali kupambana kusogeza huduma ya maji kwa jamii Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 40 tu ya watanzania waishio vijijini wanaopata maji, huku zikiwataja wanawake na watoto kuwa makundi yanayotaabishwa na uhaba huo

 

Alisema ili kuhakikisha kuwa kero hiyo inakwisha tayali ameanzisha harambee kwa wanananchi wa Kijiji cha Marumba kwa kuwataka kuchangia walau Shilingi 5000 kwa kila mmoja wao ili fedha zikipatikana aweze kupeleka mtu wa kuwachimbia walau Visima  Virefu Viwili ili kuwapunguzia Kadhia hiyo.

 

  

 mwisho

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close