ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

SOKO LA MBAAZI LAMKOROGA UBONGO MKURUGENZI

By

on

Na Steven Augustino, Tunduru

MKURUGENZI mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Abdallah Mussa amekiri kuchanganywa na zoezi la upatikanaji wa Soko la Uhakika kwa wakulima kuuza mbaazi zao.

Mussa alibainisha hayo wakati akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake na kwamba kutokana na kukosekana kwa soko la mazao hayo hivi sasa wakulima wanalazimika kuuza Mbaazi zao kwa bei ya shilingi 200 kwa kilo moja bei ambayo alisema kuwa inalenga kuigombanisha serikali na Wananchi wake.

Akifafanua taarifa hiyo alisema miaka yote wakulima wa halmashauri yake walikuwa wakitegemea Soko kubwa la kuuza mbaazi kwa wanunuzi kutoka Nchini INDIA ikiwa ni toauti na msimu huu.

Alisema katika kufuatilia upatikanaji wa soko hilo ofisi yake ilibaini kuwepo kwa Tangazo ambalo lilitolewa na Serikali ya Nchi India kusitisha ununuzi wa zao hilo mwaka huu katika nchi ya Tanzania.

Alisema hata hivyo ofisi yake ilijitahidi pia kufanya mawasiliano na  Mnunuzi mkubwa wa wilaya ya tunduru kampuni ya Export Trading Compun Ltd Delsh Poujary ambaye alikuwa tegemeo katika ununuzi wa mazao hayo aliwaeleza kuwa hadi sasa bado alikuwa hajatumiwa fedha za kuanza ununuzi huo kutoka kwa mwajiri wake.

Aidha Mkurugenzi huyo pia aliwaonesha Waandishi wa Habari Nakala ya Gazeti la Nchi ya India la Tarahe 5 Agosti mwaka huu lililoeleza kuwa mwaka huu wananunua mbaazi  ndani ya nchi yao kwanza na kama kutakuwa na mahitaji zaidi ya mbaazi watanu wigo na kwanda kununua katika nchi za Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Hata hivyo waliwatuhumu baadhi ya wanunuzi ambao wamekuwa wakipeleka maombi ya kutaka kununua mbaazi kutoka kwa wakulima lakini wamekuwa hawatekelezi makubaliano hayo.

Kampuni ya S& Magro EnterPrises aliahidi kuwa Mbaazi za mwaka 2017/2018 kwa bei ya 865 hadi sasa hawajafika na kuanza kununua.

Alisema kutokana na kadhia hiyo hadi sasa hakuna mnunuzi aliyejitokeza kwenda kununua Mbaazi kutoka kwa wakulima wa mazao hayo zaidi ya wanunuzi wadogo wadogo jambo linalo tishia halmashauri yake kukosa mapato kutokana na mazao hayo.

Aidha katika taarifa hiyo Musaa alieza kuwa ,Msimu wa  2016/2017 halmashauri ilipata ushuru milioni 146 kutokana na zao hilo.

 Alisema kufuatia hali hiyo kwa sasa Halmashauri yake inafanyaa mawasiliano na Viongozi na Watendaji wake katika katika Vijiji, Kata na tarafa zake zote kwa kutoa maelekezo ya kufanya maandalizi ya kutenga maeneo ya kuuzia mazao mchanganyiko ikiwemo mbaazi.

Kwa  mujibu wa Waraka wa utambuzi wa mazao ya Biashara uliotolewa kwa makatibu tawalaa wa Mikoa na kuasainiwa na katibu Mkuu tamisemi

Eng. Mussa Iyombe wa julai mwaka huu mbaazi zimetajwa kuwa mazao yote ya jamii ya Nafaka ikiwomo Mbaazi, mahindi, karangaa ni mazao ya chakura.

Kwa mujibu wa walaka huo Mazao ya Biashara ni Pamba, Kahawaa Korosho, chai, Zabibu, Alizeti, Tumbaku, katani/ Mkonge, Miwa Mauwa, Nazi, Pareto, Kokoa, Mchikihi au mawese na Ufuta.

Hata hivyo mkurugenzi huyo alishushia lawama Bodi ya mazao mchanganyiko kutokuwa na meno tatizo analo liona ni Bodi ya mazao mchanganyiko kutokuwa na meno.

Wakiongelea kadhia hiyo kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wa mzazo hayo walisema kuwa kutokana na kukosa soko la uhakika la kuuzia mbaazi zao wamekata tama hata ya kuvuna mbaazi zao kutoka mashambani.

Mwisho

 

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close