ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

RC MTAKA: VIONGOZI WA DINI NA WATANZANIA TUENDELEE KUMUOMBEA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.

on

Na Ismail Ngayonga MAELEZO

Dar es Salaam

4.12.2016

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewata Viongozi wa Dini na Watanzania kuendelea kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kurejesha misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Anasema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Utawala wa Rais John Pombe Magufuli, Serikali ya Awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo katika kupiga vita rushwa, ufisadi na kusimamia nidhamu na miiko ya Uongozi katika utumishi wa Umma.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kuelekea katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara.

“Ndani ya Rais Magufuli anaonekana, Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kukemea hadharani vitendo vya uvunjifu wa maadili ya mtumishi wa umma ikiwemo rushwa na ufisadi” anasema Mtaka.

Kwa mujibu wa Mtaka anasema hatua zinazoendelea kuchuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ni jambo la kupongezwa, kwa kuwa limelenga katika kuwakumbusha watendaji kuwa Uongozi ni dhamana.

Alisema kuwa hatua zinazochuliwa na Rais John Pombe Magufuli, zinaendelea kuongeza heshima ya Viongozi wa Tanzania katika medani ya kimataifa ya kusimamia nidhamu, maadili na miiko ya Uongozi ambayo imetekelezwa katika kipindi chote cha miaka 55 ya uhuru.

Anaongeza kuwa, hatua hizo zilizofikiwa na Viongozi hao ni changamoto kwa Viongozi Vijana waliopo nchini kuendelea kuheshimu misingi iliyoachwa na waasisi wa taifa, na hivyo kuiwezesha Tanzania kuendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo katika siku za usoni.

Mtaka alisema Kiongozi wa Umma ni kioo na kiunganishi katika jamii anayoiongoza, hivyo ni wajibu wa kila kiongozi wa umma kujenga taswira chanya ya kiutawala katika kuwahudumia wananchi kwa kutambua kuwa dhamana ya kiongozi ndio tumaini la watawaliwa.

“Katika siku za hivi karibuni tumeshudia sekta binafsi zikichukua watumishi waaandamizi kutoka Serikalini, hiki ni kiashiria kuwa nidhamu na maadili ya kazi yameimarika kwa kiasi kikubwa sana Serikalini” alisema Mtaka.

Akifafanua zaidi Mtaka alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Awamu ya tano pamekuwepo na mageuzi makubwa katika utendaji na uwazi wa shughuli mbalimbali za Serikali, hatua iliyosaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikipotea katika miaka ya nyuma.

MWISHO   

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

Close