ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

SIASA

Rais Mugabe kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri

By

on

Rais wa Zimambwe Robert Mugabe anatarajia kufaya mabadiliko katika baraza la mawaziri wiki ijayo.

Kwa mujibu wa habari,rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 anatarajia kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri hasa baada ya migogoro ya hapa na pale kati ya wagombea wa nafasi ya urais.

Emerson Mnangagwa mwenye umri wa miaka 76 ambae ni makamu wa rais ameshutumiwa na mke wa rais kuwa ana njama za kumpindua Mugabe.

Rais Mugabe ametangaza kuwa wiki ijayo lazima afanye mabadiliko katika serikali ambapo baadhi ya wafanyakazi wanaweza kufutwa kabisa.

Ripoti zinaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Mnangagwa kuchukua nafasi ya urais kupitia chama cha Zanu.

Mwisho Rais Mugabe alifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri Septemba 2015.

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close