ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

MWENYEKITI,KATIBU WA CHAMA WANUSURIKA KIFO

By

on

NA  Yeremias  Ngerangera……Namtumbo
Mwenyekiti  wa  chama  cha  mapinduzi  wilayani  Namtumbo mkoani  Ruvuma  bwana  Benjamini  Nindi ,Katibu  wa chama hicho  Joyce  Mwenda  w amenusurika kifo  jana  baada  ya  gari  ya  chama kuacha  njia  na kupinduka  katika kijiji cha Ligera  wilayani  humo.
Gari  yenye  namba  T640 BEU Mali ya chama  cha Mapinduzi  wilayani  Namtumbo  ilianguka katika kijiji  hicho kutokana  na mwendokasi  ambapo   dereva  wa  gari  hiyo  bwana  Burkadi  Ngonyani alishindwa  kuimudu  kona iliyopo  katika  pacha  ya kuelekea  kijiji  cha Ulamboni  na kijiji cha Ligera .
Mtendaji  kata  wa  kata  ya Ligera bi  Lidia Mpombo  alisema  kuwa gari  hiyo ilianguka kutokana  na mwendokasi  na kumfanya dereva  wa gari  hiyo ashindwe  kumudu kona  iliyopo katika  pacha za barabara   iendayo  kijiji cha ulamboni  na ligera hali  iliyomfanya  dereva huyo  kulazimisha  hali iliyoifanya  gari  hiyo kupinduka  na kuanguka pembeni  mwa barabara  kuelekea kijiji  cha Ligera.
Aidha  bi  Mpombo  aliongeza  kuwa  watu  waliohusika  katika  gari  hiyo  walikuwa 8 ambapo  ni Mwenyekiti  wa  chama cha mapinduzi  wilayani Namtumbo Benjamini  Nindi,Katibu wa chama  bi.Joyce  Mwenda ,Katibu  Mwenezi  wa  chama  wilaya Bwana Kassimu  Gunda  pamoja  na Katibu  wa umoja  wa wanawake  Bi. Anna  Ndumbaro
Wengine  waliohusika kwenye  ajali hiyo  ni katibu  wa Mbunge Kalela  Amimu ,katibu  wa chama kata  ya Lisimonji  ambapo jina lake halikutambulika mara moja pamoja  na Dereva  wa gari hiyo  bwana Burkadi  Ngonyani.
Kwa  mijibu  wa Mtendaji  kata huyo  majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa  katika zahanati  ya misheni  ligera  kwa matibabu  ya awali  na baada  ya  hapo majeruhi  waliondolewa  na kukimbizwa  kituo  cha  afya  Namtumbo.
Emily  Lihawa mganga mkuu wa wilaya alithibitisha kupokelewa  kwa wagonjwa  hao na  kusema  kuwa  hali ya wagonjwa  5 kati  ya Nane  walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi  majumbani  kwao  na  wengine  watatu  ambao ni mwenyekiti wa chama ,katibu wa chama  na katibu wa umoja wa wanawake wamesafirishwa  hospitali  ya Rufaa  Songea  kwa  uchunguzi zaidi wa afya zao
MWISHO.
Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close