ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

MLIPUKO WA BOMU WAUA WATATU NCHINI COLOMBIA

By

on

Wanawake watatu wameuwawa, katika kile wakuu nchini Colombia wanasema kuwa, shambulio la kigaidi katika mji mkuu Bogota.

Mlipuko huo ulitokea katika soko moja la biashara la Zona Rosa, katika mji mkuu Bogota.

Watu wengine 11 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Meya wa Bogota, Enrique Penalosa, amesema kuwa mmoja wa wanawake aliyefariki anatoka Ufaransa.

Wakuu wanaamini kuwa mlipuko huo ulitokea ndani ya choo cha wanawake, baada ya bomu dogo kulipuka.

Mlipuko huo ulitokea Jumamosi alasiri wakati wa shughuli nyingi, katika soko hilo la kibiashara, pale lilikuwa limejaa wateja, waliokuwa wakinunua bidhaa za siku kuu ya kina baba Duniani– ambayo inasherehekewa leo siku ya Jumapili, Juni 18.

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close