ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

ELIMU

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO ATOA MAAGIZO MANNE KUTEKELEZWA, IKIWEMO KUJENGWA KWA MADARASA NANE SHULE YA MSINGI UBUNGO PLAZA

By

on

Na Mathias Canal, Dar es salaam
 
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 19, 2017 ameagiza
kujengwa madarasa nane mapya katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Jijini
Dar es salaam kutokana Na uchakavu wa Majengo ya madarasa yaliyopo sasa.
Ametoa agizo hilo katika mkutano wake na uongozi wa shule hiyo ukiwajumuisha
mtendaji na wajumbe wa mitaa,walimu na wananchi  ambao waliohudhuriwa
katika viwanja vya  shule ya Msingi Ubungo Plaza.
Mhe Makori amesema kuwa ili kuboresha elimu katika Wilaya ya Ubungo ni wazi
kuwa ni lazima kuwe Na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wanapokuwa
darasani kwa ajili ya masomo kwani ubovu wa Majengo ya shule,ubovu na
uhaba wa vyoo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wanafunzi kufeli
kutokana na kutokuwa Na miundombinu rafiki.
Alisema kuwa Kodi zinazokusanywa Na serikali kwa wananchi ni kwa ajili ya
kuwaimarishia miundombinu kuboresha afya, na Elimu hivyo serikali ni
lazima ishughulikie na Kusimamia shughuli zote ikiwemo Ujenzi wa
madarasa kwa manufaa ya wanafunzi Na wananchi kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ametoa maagizo hayo Wakati akijibu Risala iliyosomwa Na Mkuu
wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza Bi Theresa Masaba ambayo ilibainisha
changamoto nyingi ikiwemo Ukosefu wa Vyoo Bora, Ukosefu wa Uzio,
Uchakavu wa Majengo ya shule, Upungufu wa Majengo (Ofisi ya Walimu,
Darasa la awali Jiko, Maktaba), Maji taka kuelekezwa kwenye eneo la
shule, Eneo la shule kufanyika kama sehemu ya kuvutia bangi Wakati wa
jioni na siku za Wikendi sambamba na Upungufu wa samani za shule.
Mhe Mkuu wa wilaya ameagiza pia kuvunjwa kwa Vyoo vilivyopo Na kujengwa
Vyoo vingine vipya sambamba na kujengwa kwa  uzio wa shule ili kuepuka
kadhia ya watu wanaotumia kama Eneo la kuvutia bangi Na vitendo vingine
viovu visivyo kubalika katika jamii.
Aidha amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha anawakamata watu wote
wanajihusisha Na uvutaji bangi katika Eneo la shule kwani Jambo hilo
halikubaliki si tu Na shule hiyo Bali Na serikali kwa ujumla.
Sambamba Na hayo pia Mkuu wa wilaya ameagiza kuvunjwa kwa ukuta wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) ambapo Uzio wake umejengwa ndani
ya Eneo la shule.
Alisema kuwa Kanisa hilo tayari lilishapewa Notisi ya siku Saba tangu Mei 8 mwaka huu kwa ajili
ya kuvunja ukuta huo lakini hawakufanya hivyo.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Walimu Na wanafunzi wa shule,
Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza Ndg Ramadhani
Maughuu amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutembelea shule hiyo Na
kutatua changamoto hizo zilizokuwa zinaikabili shule hiyo kwa muda
mrefu.
Maughuu ametoa pongezo zake pia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C.
Makonda kwa ufanisi Na uchapa Kazi wake sambamba Na pongezi kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa
weledi Na ufanisi wa kuwahudumia watanzania Na kauli mbiu ya HapaKaziTu.
Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close