ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

MFUMUKO BEI YA SULPHUR WATISHIA UZALISHAJI WA KOROSHO TUNDURU

By

on

Na  Steven  Augustino, Tunduru

MFUMKO wa Bei ya Dawa ya kuzuia Ugonjwa wa Ubwiriunga katika Mikorosho kwa Wakulima  wa zao hilo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma umeibua hofu ya kushindwa kuhudumia zao hilo hali itakayo pelekea kushuka kwa mavuno ya Korosho katika msimu wa mwaka 2017/2018.

Hofu hiyo imetokana na kuwepo kwa mfumko  mkubwa wa Bei ya dawa  aina ya sulphur ya unga ambayo hutumika kupulizia kwa ajili ya kukinga mikorosho yao isiharibiwe  na Ugonjwa huo hatari katika mikorosho yao.

Wakifafanua taarifa hiyo kupitia mahojiano maalumu,wakulima hao walisema kuwa Bei ya Sulphur kwa mwaka huu ni kati ya shilingi 60,000/ hadi 80,000/=  kwa mfuko mmoja ikilingwanishwa na Bei kati ya shilingi 15,000/= hadi 20,000/= kwa mfuko huo katika kipindi cha simu wa kilimo wa mwaka 2016/2017.

Akifafanua taarifa hiyo Hasan Mohamed wa Kijiji cha Mkonda alisema kuwa mbali na Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kugawa Bure madawa hayo kwa wakulima lakini kumeonesha kuchochea ukubwa wa bei ya madawa hayo jambo ambalo walidai kuwa ni hatari kwa zao lao.

Alisema kutokana na kupanda kwa bei hiyo hivi sasa wakulima wengi wameanza kuuza mali zikiwemo Pikipiki na Nyumba walizo wekeza baada ya kuuza Korosho zao katika  msimu uliopita ili waweze kununua Sulphur kwa ajili ya kuhudumia mashamba yao.

Naye  Bw. Said Kambutu mkulima wa Kijiji cha Mhuwesi kwa upande wake  ameishauri Serikali kuangalia utaratibu mzuri zaidi wa kuingiza na kusambaza madawa hayo ili kuwabana wafanyabiashara hao ikiwemo utaratibu wa kutoa Bei elekezi kwa ajili ya kuuzia madawa hayo.

Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia  Usambazaji  na ugawaji wa Madawa hayo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pamoja na kukiri kuwepo kwa upungufu wa Sulphur hiyo alisema kuwa tayali Wilaya yake imekwisha pokea mgao wake  kwa asilimia 98% na kuzisambaza kwa wakulima waliokuwa wameainishwa kupatiwa mgao wa kati ya mfuko mmoja au miwili kwa kila mkulima.

Alisema Wilaya ya Tunduru ilipangiwa mgao wa Tani 1000 na kwamba tayali Tani 998 zimekwisha pokelewa na kusambanzwa kwa wakulima na kwamba taarifa alizo kuwa nazo kiasi kilicho baikia kimekwisha pakiwa kwenya magari katika bandari ya Mtwara tayali kupelkwa Wilayani Tunduru.

Kuhusu upungufu wa dawa hiyo alisem kuwa hali hiyo imetokana na wafanyabiashara wengi wa Sulphur kuogopa kuagiza dawa hiyo baada ya kupata taarifa kuwa Msimu huu Serikali itatoa dawa hiyo Bure kwa wakulima wake.

Afisa Kilimo wa Wilaya ya Tunduru  Chiza Malando alisema kuwa takwimu za mahitaji ya Sulphur kwa wakulima wa Wilaya ya Tunduru ni Tani 5000 kwa mwaka na kwamba Sulphur iliyofika awamu hii ni wastani wa asilimia 1% ya mahitaji yao dawa ambazo ni kidogo mno hali ambayo inaonesha kutishia kushika kwa uzalishaji wa Zao hilo katika msimu ujao wa mavuno ikilinganishwa na mavuno ya Tani Elfu 14.7 katika msimu uliopita wa mwaka 2016/2017.

Alisema kuwa kutokana na uhaba huo tayali  ofisi yake imeanza kutoa elimu kwa wakulima wake kujipanga na kuanza kutumia madawa maji yanayo onekana kuuzwa kwa bei nafuu ili kunusuru mazao yao yasihalibiwe na wadudu pingamizi wa Mikorosho.

Wakati hayo yakiendelea uchunguzi unaonesha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa Sulphur wameonekana kutumia upungufu wa dawa hiyo kwa kuwaumiza wakulima kwa kuwakopesha mfuko mmoja wa Sulphur kwa makabaliano ya kulipwa Gunia moja la kilo 100 za Korosho wakati wa mavuno hayo.

Mwisho

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close