ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

SIASA

Mahakama yavunja kikao cha Bunge la Catalonia juu ya uhuru

By

on

lhamisi hii Mahakama ya Uhispania imevunja kikao cha bunge kiliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu (Oktoba 9) katika Bunge la Catalonia kuhusu matokeo ya kura ya maoni kuhusu kujitawala kwa eneo hilo.

Kura ya maoni ambayo serikali imeitaja kuwa ni kinyume cha chera. Suala la uhuru wa Catalonia lingezungumziwa katika kikao hicho.

Uamuzi huo umechukuliwa kwa haraka na kwa kauli moja na majaji wa Mahakama ya Katiba,a mbayo ilitangaza kuwa kura hiyo ya maoni ilikua kinyume cha sheria.

Wakati huo huo serikali ya Uhispania imesema haitakubali vitisho kutoka kwa viongozi wa eneo la Catalonia.

Tayari kiongozi wa Catalan amesema kuwa wiki ijayo, atatangaza uhuru wa eneo hilo.

Serikali ya Madrid inasema, haitambui kura hiyo ya maoni na ni sharti viongozi wa eneo hilo wafuate sheria kabla ya kufanyika kwa mazungumzo yoyote.

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close