ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

BURUDANI

HUSSEIN MACHOZI ASIMULIA ALIVYOFUMANIWA NA MKE WA MTU NA KISHA KUPEWA KICHAPO NCHINI KENYA

By

on

Msanii Hussein Machozi ambaye sasa amerudi nchini kutoka nchini Italia amefunguka na kusimulia kisa chake cha kufumaniwa alivyokuwa Kenya na kusema kuwa kama asingekimbia huenda mambo yangekuwa mabaya kwake.

Hussein Machozi amesema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa yeye alikwenda Kenya kikazi na mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye alikuwa ni binti aliyeandaa show yake Kenya, hivyo alipofika alimpokea Airport na kwenda naye hotel.
“Kwa hiyo tulipofika hotel tulikuwa tunapanga mipango ya hapa na pale, kumbe yule binti ana mshikaji wake ambaye ana wivu sana na yeye, hivyo yule jamaa alikuja na magari kama mawili yakiwa na mabaunsa kibao.
“Wakatuzunguka pale na kuanza kunipiga vibao ila nashukuru Mungu kuna baunsa mmoja pale pale alinishtua na kuniambia nikimbie, hivyo niliruka ukuta wa hotel na kukimbia.
“Kwa hiyo wale wahudumu pale ndiyo walianza kusambaza habari kuwa nimefumaniwa ila nisingekimbia huenda ingekuwa mbaya kwangu” alisisitiza Hussein Machozi
Mbali na hilo Hussein Machozi anasema alimua kwenda nchini Italia baada ya kuona muziki unampa mawazo hivyo Mungu akamfungulia mlango  mwingine na kuamua kusepa huko, ambako anadai anasoma na kufanya shughuli zingine zinazomuingizia kipato.
Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close