ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MCHANGANYIKO

DC HOMERA AHIMIZA UANZISHWAJI WA MFUKO WA ELIMU KUNUSURU WATOTO MASIKINI I

By

on

Na Steven Augustino, Tunduru

MKUU wa Wilayanya Tunduru mkoani Ruvuma JUma Homera amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuinginza mpango wa uanzishaji wa mfuko wa Elimu ili fedh zitakazo patikana ziweze kusaidia kusomesha watoto wasiokuwa na uwezo.

Dc, Homera alisema hayo wakati akiongea na wananchi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mlingoti mjini hapa na kwamba mfuko huo ambao utakusanya fedha kutoka katika mazao mbalimbali unaweza kuwa mkombozi kwa watoto hao pamoja na kusaidia kujenga miundombinu ya shule.

“Tunduru ni Wilaya tajiri, inalimaa mazao mengi ikiwemo Korosho, Mpunga, Mihogo na jamii za Mikunde” alissema Dc, Homera na kwamba endapo utaandaliwa utaratibu mzuri waa kuyaauzaa mazaao hayo naa wakulima wote kuchangia mfuko huo utapataa fedha nyingi na kuiletea maendeleo wilaya yetu

Aidha katika hotuba hiyo pia Dc, Homera pamoja na kukemea Jeshi la Polisi na Mahakama Wilayani humo kwa kuto tenda haki pindi inapo tokea matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa aliwataka watoto wenye malalamiko kuyapeleka moja kwa moja ofisini kwake ili aweze kuchukua hatua za haraka kwa wahusika.

 Mweneyekiti wa halmashauri ya Wilaya  hiyo Mkwanda Sudi alisema ili kufikisha ujumbe wa maadhimisho hayo kwa watu wengi kwa wakati mmoja aliwashauri  Walimu wa shule zote wilayani humo kuwaandikia Barua wazazi na walezi za kuwataka kufika katika maadhimisho hayo mwakani.

Awali akisoma risala ya maadhimisho hayo, Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Jamuhuri Sara Daniel alisema kuwa katika kipindi cha January hadi April mwaka huu jumla ya watoto 25 waliokolewa wakiwemo 15 waliozaliwa nje ya ndoa na 20 waliozaliwa katika ndoa walilipotiwa kutelekezwa na wazazi wao.

Alisema sambamba na kutelekezwa kwa watoto hao pia watoto 27 wakiwemo watoto wanzao 12 ambao walikamatwa wakiwa wanasafirishwa kwenda Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kutumikishwa na wengine 15 walisaidiwa matibabu baada ya kufanyiwa ukatili wa kingono katika kipindi hicho.

Mwisho

 

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close