ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

AFYA

Cuba Yaipongeza Muhimbili Leo kwa Kutoa Huduma Bora

By

on

Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo akizungumza na baadhi ya wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati akiitembelea leo. Kushoto ni Mratibu wa madaktari wa Cuba nchini, Dk Maylen Lopez. Kutoka kushoto wa tatu ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Muhimbili, Makwaia Makani, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk. Julieth Magandi, ofisa Idara ya ufundi, Mkurugenzi wa Tiba, Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru na  Mkurugenzi wa Ufundi, Gaudence Aksante.

0002

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi, Gaudence Aksante.

0003

Balozi wa Cuba nchini, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru leo kabla ya kutembelea maeneo ya kutoa huduma katika hospitali hiyo.

0004

Balozi wa Cuba na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU)

0005

Ujumbe kutoka Ubalozi wa Cuba ukiwa katika chumba cha upasuaji Muhimbili leo.

0006

Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja na ubalozi wa Cuba leo baada ya kuitembelea hospitali hiyo. 

 PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

………………….

Na John Stephen

Balozi wa CUBA nchini ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo na kuipongeza hospitali hiyo kwa kutoa huduma nzuri za afya.

Ujumbe kutoka ubalozi huo umetembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma, ikiwamo vyumba vya kutoa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), vyumba vya upasuaji na maeneo mengine ya kutoa huduma.

Hospitali hiyo inashirikiana na Cuba katika kutoa huduma ya afya na imeahidi kuendelea kushirikiana na MNH kwa ajili ya kuboresha huduma hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema hospitali hiyo itaendelea kushirikiana na Cuba ambayo imeahidi kupeleka wataalamu wake katika hospitali hiyo.

 “Tunaushukuru ubalozi wa Cuba kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha, hii ni moja ya njia nzuri ya kutekeleza malengo yetu,” amesema Profesa Museru.

Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Profesa Lucas Domingo Hernandez Polledo ameipongeza Muhimbili kwa kufanya upanuzi mkubwa katika majengo mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora.

“Nimefurahishwa na huduma bora, pia vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalimu ni vizuri na vimekizi mahitaji ya wagonjwa,” amesema Balozi Polledo.

Naye Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk Julieth Magandi amesema Cuba imekubali kuipatia Muhimbili wauguzi waliobobea katika kutoa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

“Cuba imekubali kuipatia Muhimbili madaktari wawili waliobobea katika kutoa huduma za uzingizi, madaktari bingwa wawili wa kutoa huduma katika vyumba vya upasuaji na daktari bingwa mmoja wa mionzi,” amesema Dk Magandi.

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close