ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

MITANDAONI

BEYONCE AJIFUNGUA MAPACHA

By

on

Ni nyakati za furaha kwa wapenzi/wanandoa Beyonce na J-Z baada ya kuwakaribisha mapacha wao wachanga kabisa mwishoni mwa wiki hii. Gazeti la US Weekly liliripoti.

Kulikuwa na siku za mijadala katika mitandao ya kijamii kuhusu kujfungua kwa mwanamuziki nguli mwenye miaka 35 katika kituo kimoja cha afya huko Los Angeles nchini marekani. Mdogo wa mwanamziki huyo, Solange Knowles alionekana akirandaranda kwenye kituo hicho cha afya, ndipo mapaparazi walipojisogeza ili kufahamu undani wa jambo hili.

Mwanzoni mwa mwaka huu mwanadada huyu alipiga picha mbele ya ua kubwa huku kashikilia tumbo lake na kupost kwenye ukurasa wake wa instagram kwamba wamebarikiwa kwa kutarajia kuleta zawadi nyingine.

Supastar wa miondoko ya Hip Hop Jay Z, mwenye miaka 47 Jumanne iliyopita alionekana akiondoka kwenye kasri lao lililopo Beverly Hills na kuelekea kwenye kituo hicho cha afya na mara ulinzi katika kituo hicho uliimarishwa.

Mapacha hawa wanaungana na Blue Ivy, binti wa wapenzi hawa mwenye umri wa miaka mitano.

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close