ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

BURUDANI

BAADA YA POST YA GWAJIMA, DIAMOND PLATNUMZ AMUANDIKIA ‘CHONDECHONDE’

By

on

Hazijafika saa 72 toka mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz aachie wimbo mpya ambao unagusia yanayoendelea sasa hivi Tanzania ambapo baada ya Askofu Gwajima kuusikia, alitumia time yake kupost kwenye Instagram yake haya maneno hapa chini.

Baada ya Diamond Platnumz kuona post hiyo ya Askofu Gwajima ameyaandika yafuatayo >>> “Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba?….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima

Nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza na wote kufurahi kwa pamoja

Lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi? chondechonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho ?, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima???”

Facebook Comments

You must be logged in to post a comment Login

Close